Ufaransa : Macron na Le Pen watagombea kiti cha urais

Emmanuel Macron amechukua nafasi ya kwanza, akafuata Marine Le Pen kwenye uchaguzi wa siku ya jumapili tarehe 10 Aprili 2022. Hao wawili, waliopata kura nyingi zaidi ya wengine wagombea, watawania nafasi ya rais katika duru ya pili ya uchaguzi huo.

Tarehe 24 Aprili, duru ya pili ya uchaguzi itafanyika nchini Ufaransa. Katika duru ya kwanza ya hii jumapili, rais wa Ufaransa, ambae ni mwanachama wa La République en Marche, Emmanuel Macron amepata 27,6% za kura. Amepigiwa kura na watu zaidi ya miliyoni tisa na nusu. Nafasi ya pili imechukuliwa na Marine Le Pen, wa chama Rassemblement National amepata 23,41% za kura. Mwanamama huyo amepigiwa kura na watu zaidi ya miliyoni nane. Mgombea aliechukua nafasi ya tatu ni aitwae Jean Luc Mélenchon wa chama La France insoumise aliepata kura 21,95%. Amepigiwa kura na watu zaidi ya miliyoni saba na nusi. Wengine wagombea waliwojichagulisha lakini wakapata kura chache ni pamoja na Eric Zémmour, Valérie Pécresse, Yannick Jadot, Jean Lassalle, Fabien Roussel, Nicolas Dupont-Aignan, Anne Hidalgo, Philippe Poutou na Nathalie Arthaud.

Emmanuel Macron na Marine Le Pen walikua waliwania nafasi ya urais kwenye duru ya pili ya urais mwaka 2017. Kipindi hicho, Emmanuel Macron alijipatia ushindi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *