Burundi: Maisha ya chifu-imbonerakure yako hatarini sana

Amelazwa tangu takriban wiki moja sasa kwa hali ya kukosa fahamu katika Hospitali ya Prince Régent Charles. Kiongozi wa imbonerakure wa kata ya Kigwati kitongoji cha Nyakabiga anadaiwa kumchokoza mfanyakaza wa Idara ya Ujasusi na kudaiwa kumvunjavunja. Awali, ilikuwa doria ya imbonerakure usiku wa manane wa jumanne kuamkia jumatanu wiki jana. Vyanzo vyetu vya habari vinaamini kuwa endapo kiongozi huyo wa imbonerakure ya Kigwati Ladeck akifanikiwa kunusurika itakuwa ni miujiza. (Le Mandat)

Katika chumba cha pamoja nambari 36 cha Hospitali ya Prince Régent Charles, anayejulikana kama Ladeck hajitikisi tena kulingana na mashahidi. Imbonerakure huyu, ambaye ni mmoja wa watoza ushuru wa ofisi ya Meya wa jiji la Bujumbura, haongei pia. Huku bandeji zikiwa zimezungushiwa fuvu kichwani upande wa kulia, kiongozi wa vuguvugu la vijana wa chama CNDD-FDD kutoka Kigwati amelishwa kwa njia ya mishipa kwa siku chache katika chumba hicho chenye vitanda sita. Baadhi ya wanachama kutoka chama tawala Nyakabiga na maafisa wa polisi waliovalia kiraia humtembelea mara kwa mara, kulingana na vyanzo vyetu.

Yote yameanza wakati wa doria ya usiku

Imbonerakure wawili kutoka Kigwati na kiongozi wao Ladeck wamekutana na Petit wakati wa doria katika kata ya Nyakabiga ya 3, kwa usahihi zaidi kwenye barabara ya 10. Ilikua karibu saa nane usiku. Petit, meneja wa baa “La diffusion” iliyoko kwenye barabara ya tano katika kata ya Nyakabiga ya 3 mkabala na kampasi ya Mutanga ya Chuo Kikuu cha Burundi, alikua chini ya mita kumi kutoka nyumbani kwake. Alikua amerudi, kama kawaida, baada ya kuondoka kwa mteja wa mwisho wa biashara ya baba yake, ambae ni mustaafu kutoka jeshini. Imbonerakure hao watatu wakiwa wamebeba fimbo ndefu walimkamata na kuanza kumpiga kwa mujibu wa Petit mbele ya mkuu wa kata ya Nyakabiga 3. Vyanzo vyetu vinaeleza kuwa Petit alifanikiwa kukimbia na kuelekea barabara ya 9 na kuanza piga kelele za kuomba msaada mbele ya lango la mkuu wa kata ya Nyakabiga 3 Bonaventure Ndayishimiye. Petit amemweleza mkuu wa wilaya hiyo na wakazi wengine wa kata hiyo ambao wametoka nje ya nyumba zao kuwa hajui ni kwanini watu hao watatu wanamfukuza. “Alikuwa karibu kupanda ukuta. Lazima tumufunze adabu, “amejibu mmoja wa imbonerakure kulingana na mashahidi. Licha ya majaribio kadhaa, chifu wa kata hakuweza kuwashawishi imbonerakure kuondoka, kulingana na vyanzo vyetu.

“Afisa wa ujasusi” na polisi

Mtu ambaye amehisiwa kuwa Mfanyakazi wa Idara ya Ujasusi alipita sehemu hiyo akiwa na polisi, kwenye gari, huku mabishano yakiendelea. Baada ya kuwanyang’anya fimbo waliyoitumia kwa zamu imbonerakure hao kumpiga yeyote aliyethubutu kumutetea Petit, “mfanyakazi wa idara ya ujasusi” alionekana mwenye hasira. Imbonerakure pia walikua na hasira. “Kila wakati, chifu wa kata Bonaventure na afisa wa polisi walikua wakituliza hali wanapojaribu kupigana”, anaripoti shahidi. “Afisa wa idara ya upelelezi” aliendelea kuwaambia imbonerakure kwamba walizidi eneo lao wakati wa doria kulingana na mashahidi.

Pigo “mbaya”

Baada ya takribani saa moja ya mivutano, yule “afisa wa idara ya ujasusi” aliwaambia wote waliokuwepo pale warudi majumbani mwao kwa mujibu wa vyanzo vyetu. Petit alichukua fursa hiyo kujiondoa kwa mujibu wa vyanzo hivyohivyo. Lakini, wakati “afisa wa ujasusi” alichukua barabara ya nane kurudi nyumbani na polisi, wale imbonerakure watatu walimufuata kulingana na vyanzo vyetu. Dakika chache baadaye, Ladeck alionekana akipiga kelele kwa maumivu akiwa chini. “Baada ya dakika tano hivi, tulisikia kelele. Tulipofika eneo hilo, kichwa cha yule kijana kilikuwa na mwanya mkubwa na kilikuwa kinavuja damu nyingi. Hatujui ni nini kilitokea lakini marafiki zake wawili walikuwa wametoroka,” alisema mkazi wa Nyakabiga.

“Afisa wa idara ya upelelezi” anazuiliwa

Ilipangwa kwamba Alhamisi hii, “mfanyakazi wa idara wa Ujasusi” ahamishwe, kwa maagizo ya Afisa wa Polisi wa Mahakama ya Nyakabiga, hadi kituo cha polisi cha manispaa, BSR ya zamani. Alifungwa takriban siku tano kwenye gereza ndogo ya kituo cha polisi katika kitongoji cha Nyakabiga baada ya kukamatwa na mkuu wa kituo eneo hili lililoko wilayani Mukaza katika jiji la Bujumbura. Kwa upande wake, polisi, aliyekua akishirikian aliachiliwa na mkuu wa polisi siku ya Ijumaa, kulingana na vyanzo vyetu.

Baa “La diffusion” inafanya kazi kwa woga na meneja wake amekosekana 

Baadhi ya wafanyakazi wa baa wana hofu kulingana na vyanzo vyetu. Wanasema hawafahamu alipo Petit kwa sasa baada ya kupigiwa simu na chifu wa kitongoji cha Nyakabiga Gervais Ndihokubwayo. Vyanzo vyetu vya habari vinatuambia kuwa jicho la kulia la Petit limejeruhiwa vibaya baada ya kupigwa na imbonerakure hao watatu. Pia wanaripoti kwamba mikono yake pia ina majeraha.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari, mmiliki wa baa hiyo ya “La diffusion”, inayoishi mikoani, yuko katika mji wa Bujumbura tangu siku kadhaa kufuatilia kwa karibu hali hiyo.

Tulipowasiliana naye kwa njia ya simu, mkuu wa kitongoji cha Nyakabiga Gervais Ndihokubwaho alikataa kuzungumza chochote kuhusu faili hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *