Wakati wa kuondoa vikwazo dhidi ya BBC, Baraza la Taifa la Mawasiliano la Burundi lilitaja sababu kuu mbili. Mapendekezo ya Rais wa Jamhuri na hali ya kwamba redio ya BBC imekubali kuomba idhini mpya. Lakini, kwa kweli, sababu halisi ni utekelezaji wa ramani iliyohitimishwa kati ya serikali na Umoja wa Ulaya.
Kuimarishwa kwa uhuru wa vyombo vya habari ni mojawapo ya hoja ambazo Umoja wa Ulaya unaendelea kuibua katika fremu ya mazungumzo ya kisiasa na Burundi. Ni katika muktadha huu ambapo CNC iliidhinisha kuanzishwa tena kwa shughuli za redio BBC katika ardhi ya Burundi. Mamlaka ya Burundi pia yanapendelea uidhinishaji wa kupita kiasi wa vyombo vya habari vipya ili “kuthibitisha mageuzi katika suala la uhuru wa vyombo vya habari”. Katika sekta hii, mamlaka za Burundi bado hazioni jinsi ya “kufanya amani” na vyombo vya habari vilivyochomwa na kupigwa marufuku kitaifa. Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari, utawala wa CNDD-FDD unakusudia kuondoa hati za kukamatwa kwa wakurugenzi na baadhi ya waandishi wa habari wa vyombo hivi na kisha kutaka warejee nchini na vyombo vya habari vyenye majina mengine. Lakini, suala la hivi vyombo vya habari ambavyo viko ukimbizini ni mchakato mgumu na sio kipaumbele kwa sasa, vinaripoti vyanzo vyetu.
Vipaumbele ifikapo Juni
Kufikia Juni, mamlaka ya Burundi inapaswa kuwasilisha matokeo yanayoonekana juu ya matumizi ya ramani kwa washirika wao wa Ulaya. Hii ndiyo sababu, katika kinyang’anyiro hiki cha muda, kundi jingine la wanachama wa upinzani wa kisiasa na mashirika ya kiraia walio uhamishoni wanapaswa kurejea makwao hivi karibuni. Kulingana na vyanzo vyetu, wanatoka hasa Brussels, Kampala na Kigali. Kufikia sasa, wanasiasa hawa wanaorejea na wanachama wa mashirika ya kiraia wanakutania kwenye kitu kimoja. Walipinga rasmi muhula wa tatu wa Rais Pierre Nkurunziza lakini wakadumisha kwa uficho uhusiano mzuri na CNDD-FDD.
Faili ya “wahusika na majaribio ya kupindua serikali mwaka 2015”
Utawala pia unakusudia kupata alama kwa kuwaachilia “waliojaribu kupindua serikali mwaka 2015” na wafungwa wengine wa kisiasa. Kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa ni mojawapo ya hoja ambazo Umoja wa Ulaya unaendelea kujadiliana. Kulingana na vyanzo vyetu, ripoti ya “hao wenye walijaribu kupindua serikali” ilijadiliwa nyuma ya pazia la chama cha urais mwaka jana, 2021, lakini hakukuwa na makubaliano. Baada ya moto uliowauwa mahabusu na kuteketeza sehemu kubwa ya gereza kuu la Gitega, Rais Evariste Ndayishimiye alimtuma mjumbe kwenda kuwaeleza “wanaoshutumiwa kujaribu kupindua serikali” kwamba hawakulengwa kabisa, kinyume na “iliyosemwa mitaani,” vyanzo vyetu vinaeleza.
Kwa sasa, serikali ya Burundi inawathibitishia washirika wao wa Ulaya kwamba kila kitu kinaweza kujadiliwa lakini wanakataa kuwekewa ratiba ya kushughulikia faili kulingana na vyanzo vyetu.