Video ya Rais Magufuli ni ya 2019.

Baada ya siku kadhaa za mabishano kuhusu afya ya John Pombe Magufuli, video inayomuhusu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaonekana kwenye mitandao ya kijamii. Baadhi ya wanamtandao wanadai kuwa video hii kutoka kituo cha runinga cha Citizen nchini Kenya inathibitisha kuwa Rais John Pombe Magufuli yu hai na yuko mzima. Kwa hakika Rais John Pombe Magufuli hajaonekana hadharani kwa zaidi ya wiki mbili.

Sina nia ya kubishana kuhusu hali ya afya ya Rais John Pombe Magufuli bali najikita kwenye video ambayo niliiona ikisambaa kwenye vikundi vya Whatsapp kuanzia Machi 13, 2021.

Video ya lugha ya Kiswahili imechukuliwa kutoka kwenye kipindi cha runinga cha Citizen cha Kenya NIPASHE WIKENDI. Ili kuzindua ripoti ya Gatete Njoroge, watangazaji hao wawili wanasema: “Rais wa Jamhuri ya Tanzania amejitokeza hadharani siku moja baada ya taarifa kadhaa kusambaa kuhusu hali yake ya kiafya. Na Magufuli aliudhuria ghafla ya kuwaapisha viongozi aliowateua. Jijini Dar Es Salaam alitengamana na viongozi wa serikali na kuwahimiza kutekeleza majukumu yao bila ya mapendeleo”. Watoa mada wanabainisha kuwa Watanzania waliofuatilia mwonekano wa John Pombe Magufuli moja kwa moja, walionyesha furaha yao kugundua kuwa Rais wao yu hai.

Picha, maudhui ya ripoti hiyo na ukweli kwamba tukio hilo lilikuwa likitokea moja kwa moja kwenye vyombo vya habari vya Tanzania viliniwezesha kugundua kwa haraka kuwa ni tukio jingine. Video hiyo inahusu kujitokeza tena hadharani kwa Rais John Pombe Magufuli Oktoba 20, 2019 baada ya uvumi kuwa alihamishwa kutokana na matatizo ya moyo. Nakubali, kuna mfanano mkubwa kati ya matukio hayo mawili.

Nimepata pia Video yenyewe kwenye akaunti ya Twitter ya Citizen Kenya na kwenye Youtube

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *